About

This is where new technological investions,recent news & funny stuffs r firstly found......

Tuesday, March 19, 2013

NA HII NDIO PEN AMBAYO INAWEZA KUTOA WINO WA RANGI YOYOTE MTU ATAKAYO KUANDIKIA

Unapoambiwa teknolojia inakua,usidhani ni kwenye simu na computer tuu.! Bali ni hata kwenye vitu ambavyo unaweza ukavipuuzia.Hii ni pen iliyogunduliwa na mwanasayansi JIO SUN PARK ambayo inamuwezesha mtumiaji kuandikia rangi yoyote aitakayo kwa kunyonya{scan} rangi aitakayo kutoka kwenye kitu kingine chochote.pen hii imeundwa kwa kuwekewa kifaa kinacho gundua rangi{colour sensor}katika upande wake wa juu,kifaa hicho hugundua rangi ya kitu ambacho kimewekewa na hivyo huwa kinasafirisha rangi hiyo kwa njia ya dijitali{digital transmission} hadi sehemu ya katikati ya pen hii.Baada ya hapo, rangi hiyo iliyoletwa katika sehemu hiyo{inform of digital}hutengenezwa kwa kuchanganya wino wa blue,green na red ambao upo kwenye pen na kwahiyo ile rangi hutokea na tayari kwa kuandikia..!!! Lakini bila kusahau wahenga walivyosema 'kizuri hakikosa ubaya' pen hii ni gharama kwa sababu teknolojia yake ni mpya,na pia huwa inambidi mtumiaji kubadilisha battery na wino baada ya kipindi fulani cha utumiaji

0 comments:

Post a Comment