About

This is where new technological investions,recent news & funny stuffs r firstly found......

Friday, January 1, 2010

DIAMOND ASHINDWA KUFANYA SHOO VIZURI KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 36 YA CCM

Diamond platinumz ashindwa kuperfome vizuri katika maadhimisho ya miaka 36 ya CCM yaliyofanyika leo mkoani kigoma katika kiwanja cha tanganyika.Mpango mzima ulikuwa hivi;
hapo awali Diamond alisimamishwa ili apige shoo kabla ya rais kikwete kuhotubia ila ilishindikana baada ya speaker kutoa sauti ya kukoroma na hata baada ya kuachiwa muda wakurekebisha ilishindikana..!,hivyo ikabidi ampishe mheshiwa rais kuhotubia.na baada ya rais kikwete mwenyekiti wa ccm taifa kuhotubia,Diamond pamoja na dancers wake walipewa tena nafasi ya kuperfome, hata hivyo baada ya kuimba kidogo tu! sauti ikawa bado inakoroma na kufanya diamond aache kuimba na kuanza kuongea na DJ ili aweze kurekebisha mitambo, ambapo wanakigoma wengi walikuwa na shauku ya kuona shoo ya diamond katika maadhimisho hayo..... Na baada ya mwenyekiti wa ccm,rais kikwete kuondoka kiwanjani hapo,Diamond alijitahidi kupiga shoo japokuwa kulikuwa na sauti mbaya ya speaker.......... ....

0 comments:

Post a Comment